Sample Data-Articles

Mzumbe University invites applications from qualified Tanzanians and non-Tanzanians for admission into various degree programmes offered by the University for the 2022/2023 academic year for the third round of applications which starts from 18th September 2022 to 25th September, 2022.

The Bachelor degree Programmes are offered in three campuses namely, the Mzumbe University-Main Campus in Morogoro (MU); Mzumbe University-Dar es Salaam Campus College (MUDCCo); and Mzumbe University-Mbeya Campus College (MUMCCo).

Applicants wishing to be admitted into any of the programmes have to clearly indicate their campus preferences during their application. When selecting a study programme, it is important to pay attention to programme codes, as they signify the campus in which the programme is offered.

Applicants can make up to three choices; and that an applicant may be selected depending on his/her programme preferences and ability to compete based on academic performance. Any programme with a code starting with “MU” is offered at Mzumbe University - Main Campus; while the code starting with “MDA” is offered at the Mzumbe University-Dar es Salaam Campus College (MUDCCo) and a code starting with “MMB” is offered at the Mzumbe University-Mbeya Campus College (MUMCCo).

Mzumbe University urges all applicants to read carefully the entry qualifications provided hereunder before embarking on application to choose their preferred programmes

For more details,Click Here

Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe.Humphrey Polepole amevitaka vyuo vikuu nchini Tanzania kuchangamkia fursa lukuki zinazopatikana nchini Malawi hususani katika maeneo ya tafiti, kubadilishana wanafunzi na kufundisha lugha ya Kiswahili hasa wakati huu ambapo Malawi imeanzisha somo hilo kwa shule za msingi na sekondari.

Mhe.Polepole ametoa rai hiyo katika ziara aliyoifanya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu Morogoro na kuzungumza na Menejimenti ya chuo hicho ambapo alikipongeza kwa utendaji wake wa kuzalisha Wanataaluma nguli kwa miaka mingi na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kinapenya nchini Malawi na kuanzisha mashirikiano ya kimkakati na vyuo vikuu vilivyopo nchini humo.

“Vyuo vikongwe vina jukumu la kulea vyuo vidogo,nanyi Chuo Kikuu Mzumbe ni moja kati ya vyuo vikubwa  na wabobezi katika masuala ya Menejimenti na utawala kwa umma.Viongozi wengi wa Afrika walipita hapa, njooni Malawi muwajengee uwezo katika masuala ya tafiti na utawala bora.” Alisisitiza

Awali akimkaribisha Balozi, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.William Mwegoha alimweleza kuwa, chuo kimeendelea kufanya vizuri kwenye majukumu yake ya msingi na kwamba kutakuwa na mabadiliko makubwa zaidi hivi karibuni kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) utakaojenga miundombinu mipya na kufanya maboresho ya mitaala na hivyo kumshukuru kwa kutambua nafasi ya chuo kikuu Mzumbe katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Malawi na Tanzania

Nae Rasi wa Ndaki ya Mbeya ya Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Henry Mollel, alimshukuru Balozi Polepole kwa kuwasilisha fursa zilizopo nchini Malawi na kusema kuwa hatua hiyo imeongeza uelewa wa kutambua fursa nyingi zaidi ya zile walizokuwa wakiziona na kwamba inatoa msukumo na ari kubwa kwa Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Mbeya kuendelea na mchakato wa kuunda mashirikiano ya kimkakati waliokuwa wameuanzisha baina yao na Chuo Kikuu cha Malawi kwa kushirikiana kwa karibu zaidi na Balozi.

                     *******************************************************************************

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mhe. Humphrey Polepole (Kushoto) akilakiwa na Viongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe mara baada ya kuwasili Kampasi kuu Morogoro.Walieshikana mkono ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof.William Mwegoha.

Mhe.Balozi Polepole akizungumza na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe katika ukumbi wa Lumumba Complex Kampasi kuu Morogoro.

Wajumbe wa Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe wakimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini  Malawi Bw. Humphrey Polepole .

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Allen Mushi akitoa Shukrani kwa Balozi Polepole baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yake na Menejimenti.

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mhe. Polepole (Katikati), Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, (Kushoto) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Allen Mushi (Kulia) wakiwa wamekaa sehemu ya kusomea katika Majengo ya Hosteli Mpya za Maekani alipotembelea mradi huo baada ya kuzungumza na Menejimenti.

 

News and Updates

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top